Tunawafundisha wenyewe lakini maslahi yetu wanayapuuza- Mwalimu Rukia

Tunawafundisha wenyewe lakini maslahi yetu wanayapuuza- Mwalimu Rukia

Leo ni siku ya walimu duniani ambapo suala linalopatiwa kipaumbele ni hadhi ya walimu, mafunzo na stahili zao ili kuweza kuhakikisha kile wanachofundisha kwa watoto kinalenga kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Hata hivyo hali ya walimu katika maeneo mengi duniani bado inasalia duni wakati huu ambapo inaelezwa kuwa ili kufanikisha lengo namba Nne la SDGs la elimu kwa wote ifikapo mwaka 2030, walimu wapya zaidi ya milioni 69 wanahitajika kote ulimwenguni. Je nini kifanyike kufanikisha hilo? Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga amevinjari huko Buyenzi mjini Bujumbura nchini Burundi kuangazia hali ya walimu na kile wanachopenda kukikiona kinafanyika kuinua hadhi zao.

(MAKALA )