Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yakaribisha mchango wa Uingereza kwa huduma za wakimbizi, Uganda

WFP yakaribisha mchango wa Uingereza kwa huduma za wakimbizi, Uganda

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, nchini Uganda limekaribisha mchango wa dola milioni 21 kutoka Uingereza, amabao tayari umeleta ahueni kwa zaidi ya watoto 65,000 wanaokabiliwa na utapiamlo katika eneo la Karamoja pamoja na wakimbizi nchini humo. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Katika taairfa ya WFP, iliotolewa leo jijini Kampala, Khaim Mkurugenzi wa WFP, Uganda Mike Sackett, amesema, bila michango kama huo wasingeweza kushughulikia mahitaji ya wakimbizi haswa wakati huu ambapo idadi yao imefikia elfu sitini na sita.

Amesema kwa sasa WFP inahitaji karibu dola milioni saba kila mwezi ili ifikie mahitaji wa chakula ya wakimbizi huku gharama zikitarajiwa kupanda zaidi sanjari na ongezeko lao

Kufuatia mmiminiko wa wakimbizi hasa kutoka Sudani Kusini mnamo Agosti mwaka huu, WFP, ililazimika kukata asilimia hamsini ya mgao wa chakula kwa wakimbizi wote waliowasili Uganda kabla ya Julai 2015, ila wale wenye mahitaji ya kipekee.