Skip to main content

UNOOSA na mfuko wa amani na ushirikiano wazindua tuzo ya Shule

UNOOSA na mfuko wa amani na ushirikiano wazindua tuzo ya Shule

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya anga (UNOOSA) na mfuko wa Amani na ushirikiano leo wametangaza uzinduzi wa tuzo ya shule ya Amani na ushirikiano kwa mwaka 2017. Tuzo hiyo inaitwa “Ukiangalia nyota:Mustakhbali wa dunia”

UNOOSA inasema lengo la tuzo hiyo ni kuelimisha kuhusu masuala ya kijamii ya kimataifa miongoni mwa watoto. Wanafunzi kutoka kote duniani wanakaribishwa kuwasilisha sanaa zao zinazotanabaisha matatizo ya sasa ya kijamii na jinsi gani utafiti wa anga unaweza kuleta faida na maisha ya binadamu.

Washindi wa tuzo hiyo watatangazwa mwezi Oktoba mwaka 2017. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa UNOOSA Simonetta Di Pippo, huu ni mradi mzuri wa kujumisha sanaa na sayansi ili kuonyesha thamani ya teknolojia ya anga katika kuboresha maisha ya watu kote duniani.