Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni 249 wako hatarini kutofikia uwezo wa kimaendeleo

Watoto milioni 249 wako hatarini kutofikia uwezo wa kimaendeleo

Inakadiriwa kwamba asilimia 43 , sawa na watoto milioni 249 walio na umri wa chini ya miaka mitano katika nchi za kipato cha chini na cha wastani wako katika hatari ya maendeleo duni kutokana na umasikini uliokithiri na kudumaa. Rosemary Musumba na ripoti zaidi.

(Taarifa ya Rosemary)

"Taarifa hizo ni kwa mujibu wa mfululizo wa matokeo ya utafiti mpya wa jarida la kitabibu la Uingereza The Lancet, uitwao:kuboresha maendeleo ya utotoni kutoka sayansi hadi ukubwa wake”

Inaelezwa kuwa kuchukua hatua katika uwekezaji wa maendeleo ya utotoni kama vile kuchagiza lishe, afya, malezi bora, ulinzi na usalama na elimu ya awali, kunaweza kugharimu kiwango kidogo cha fedha cha takribani dola senti 50 kwa mtoto kwa mwaka, ukijumuisha na huduma zilizopo za afya.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO Margaret Chan uwekezaji kwa watoto wadogo ni muhimu kimaadili, kiuchumi na kijamii.

WHO, benki ya dunia na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, yamechangia na kutoa muongozo katika utafiti huo, ambao unasisitiza umuhimu wa kimataifa wa uwekezaji katika maendeleo ya utotoni.