Ingawa bado kuna changamoto Afghanistan imepiga hatua:Ban

Ingawa bado kuna changamoto Afghanistan imepiga hatua:Ban

Pamoja na zahma zinazoikabili Afghanistan, taifa hilo limepiga hatua katika kuelekea mustakhbali linaloutaka, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa ahadi ilizoziweka miaka miwili iliyopita.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moom, Jumatano mjini Brussels, Ubelgiji, kwenye mkutano maalumu kuhusu Afghanistan.

Amesema taifa hilo liliainisha mambo ya kushughulikia ikiwa ni pamoja na hatua za kukabiliana na ufisadi, mabadiliko ya mifumo ya utawala na uchumi haramu, na sasa...

(SAUTI YA BAN)

Licha ya changamoto kubwa, serikali imepiga hatua muhimu katika kuelekea kudumisha uwazi, uwajibikaji na kuboresha huduma za jamii. Napongeza kuanzishwa kwa kitucho cha kupambana na ufisadi, kuimarisha bajeti, kuongeza ushirikano na shirika la fedha duniani na kujiunga kwa Afghanistan hivi katibuni kwenye shirika la kimataifa la biashara”