Skip to main content

Kimbunga Matthew chatumbukiza watoto zaidi ya Milioni Nne hatarini

Kimbunga Matthew chatumbukiza watoto zaidi ya Milioni Nne hatarini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na serikali ya Haiti na wadau wengine kusambaza vifaa vya usaidizi kwa waathirika wa kimbunga Matthew kilichopiga Haiti hii leo.

UNICEF inasema misaada hiyo ni pamoja na vidonge vya kutakasisha maji na vya kujisafi, wakati huu ambapo watoto zaidi ya Milioni Nne wanatarajiwa kuwa wameathiriwa na zahma hiyo.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti, Marc Vincent amesema kimbunga Matthew ni kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika miongo ya karibuni na bila shaka madhara yake yatakuwa makubwa.

Kwa mantiki hiyo amesema kipaumbele ni watoto kupatiwa maji safi na salama ili kuwapuesha na magonjwa kama vile kipindupindu.