Ban alaani mashambulizi dhidi ya MINUSMA Mali

4 Oktoba 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi dhidi ya mpango wa Umoja wa mataifa nchini Mali, MINUSMA.

Kwa mujibu wa taarifa za awali mashambulizi manne tofauti yamelenga wafanyakazi wa mpango wa MINUSMA na vifaa vyake kwenye eneo la Aguelhok, mkoa wa Kidal, na kukatili maisha ya mlinda amani mmoja wa mpango huo kutoka Chad huku wengine wananane wakijeruhiwa.

Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mlinda amani huyo, serikali na watu wa Chad, na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi wote.

Ametoa wito wa kuchukuliwa hatua , ili kuwafikisha wahusika wa mashambulizi hayo kwenye mkono wa sheria, huku akikumbusha kwamba mashambulizi dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa ni uhalifu wa kivita chini ya sheria za kimataifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter