Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito watolewa kuhusu ajira bora na usalama kwenye sekta ya uvuvi:FAO

Wito watolewa kuhusu ajira bora na usalama kwenye sekta ya uvuvi:FAO

Ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za kazi katika sekta ya uvuvi imekuwa ni suala linalogonga vichwa vya habari.

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO, kazi za shuruti, usafirishaji haramu wa watu, ajira kwa watoto,usalama mdogo katika vyombo vya uvuvi na kwenye viwanda vya samaki ni masuala ambayo yamekuwa yakiarifiwa kote duniani.

Hali hii imezifanya serikali na wadau katika sekta ya uvuvi kutoa kipaumbele cha kutaka kupata suluhu ya matatizo hayo.

Na Kwa mantiki hiyo kuanzia leo Oktoba 4 wawakilishi kutoka sekta ya uvuvi, asasi za kiraia, zikiwemo jumuiya za wavuvi, wawakilishi wa serikali na mashirika ya kimataifa ikiwemo FAO wanakutana mjini Vigo Hispania ili kujadili na kupata suluhu. Uwe Barg ni afisa wa uvuvi katika shirika la FAO anaeleza nini kitarajiwe katika mkutano huo.

(SAUTI YA UWE BARG)

Tunaona ukosefu wa ajira za kutosha, tunaona fursa za ajira kwa wanawake na vijana ambazo hazitumiki, tunaona tatizo la usalama wa kijamii ikiwemo likizo ya uzazi, malipo ya uzeeni, kima cha chini cha malipo na kunahitajika mjadala, wawakilishi wa wavuvi wanahitaji kuja kwenye mjadala na kupaza sauti za wanachokipitia na wanachohitaji”