Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tiba dhidi ya kichaa cha mbwa bado ni changamoto

Tiba dhidi ya kichaa cha mbwa bado ni changamoto

Kichaa cha mbwa! Huu ni ugonjwa unaoambukizwa kwa kiasi kikubwa na mbwa na huweza kusababisha hadi asilimia 99 ya vifo kwa binadamu walioambukizwa. Hata hivyo ugonjwa huu una kinga , nayo ni kwa mbwa kupatiwa chanjo na iwapo mtu atang’atwa na mbwa basi ni lazima apate tiba ambayo ni sindano. Hata hivyo inaelezwa kuwa kuna changamoto ya kupata tiba hiyo hasa barani Afrika na Asia ambako ndiko tatizo ni kubwa zaidi. John Kibego katika makala hii ameangazia eneo la Hoima, nchini Uganda.