Janga la Lampedusa halijazuia watu kuvuka Mediteranea

3 Oktoba 2016

Miaka mitatu tangu kuzama kwa boti huko Lampedusa katika bahari ya Mediteranea na kusababisha vifo vya watu wapatao 400, bado watu wanaendelea kutumia njia hiyo kukwepa vita na umaskini na kusaka maisha bora Ulaya.

Rais wa shirikisho la msalaba mwekundu nchini Italia Francesco Rocca amesema katika taarifa ya shirika hilo kuwa hakuna mabadiliko yoyote tangu wakati huo, watu wakiendelea kupoteza maisha na huku kile wanachokimbia makwao kutopatiwa umakini.

Amesema wiki hii wafanyakazi wao waliokoa zaidi ya watu 300 kwenye eneo hilo ambao wangaliweza kupoteza maisha kama ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita.

Katika janga hilo la Lampedusa, boti ya mbao iliyokuwa na watu zaidi ya 500 ilishika moto na kuungua na hatimaye kuzama nusu maili kutoka pwani, na hivyo kuwa janga kubwa zaidi kuwahi kutokea katika bahari ya Mediteranea.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter