Skip to main content

Wananchi Colombia wakataa mkataba wa amani, Ban azungumza

Wananchi Colombia wakataa mkataba wa amani, Ban azungumza

Nchini Colombia baada ya wananchi kupiga kura na kukataa makubaliano ya amani kati ya serikali na waasi yaliyolenga kumaliza mzozo uliodumu kwa zaidi ya miongo mitano, Umoja wa Mataifa umetoa kauli ukisema kuwa ulitarajia vinginevyo. Amina Hassan na taarifa kamili.

(Taarifa ya Amina)

Wiki moja iliyopita huko Cartagena, shamrashamra zilishamiri katika utiwaji saini wa mkataba wa amani kati ya serikali ya Colombia na waasi wa FARC, takribani siku tano baadaye kura ya maoni ikatumbukiza nyongo matumaini ya amani, yaliyochochewa na jitihada za Umoja wa Mataifa.

Katika kura hiyo zaidi ya asilimia 50 wamekataa huku waliokubali ni asilimia 49.7 ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa Geneva, Uswisi akizungumza na wanahabari Geneva, Uswisi amesema..

(Sauti ya Ban)

Tungalitarajia matokeo mengine, lakini natiwa moyo na ahadi iliyotolewa na Rais Juan Manuel Santos pamoja na kamanda wa kikosi cha FARC-EP, Timoleon Jimenez”

Na kwa mantiki hiyo..

(Sauti ya Ban)

“Nimemtuma haraka mwakilishi wangu maalum Jean Arnault aelekee Havana, Cuba kuendeleza mashauriano yake.”