Madhila yanayowakabli watoto Aleppo ni ukiukwaji wa haki za binadamu: UM

3 Oktoba 2016

kuendelea kwa mashambulizi ya Serikali ya Syria na washirika wake yanayoua na kuwalemaza watoto katika maeneo ya mashariki mwa Aleppo ni ukiukaji wa kikatili wa majukumu ya kimataifa ya haki za binadamu wanayopaswa kuyaheshimu, wamesema wataalam wa Umoja wa Mataifa wa haki za watoto.

Kwa mujibu wa Benyam Dawit Mezmur nwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za mtoto, Syria na Urusi zote zimeridhia mkataba wa haki za mtoto, Zaidi ya hapo wametia saini pia sharia ya kutoshirikisha watoto kwenye vita vya silaha.

Ameongeza kuwa hii haimanishi tu kutowaingiza au kuwatumia watoto vitani, inamaanisha kutowalenga watoto wakati wa vita, kutoshambulia maeneo yao kama shule na hospitali mashambulizi ambayo yanaweza kuwa ni uhalifu wa kivita chini ya sharia za kimataifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter