Chukua msimamo dhidi ya uzee:UM

1 Oktoba 2016

Umoja wa Mataifa unaadhimisha siku ya kimataifa ya wazee kwa kuzichagiza nchi kutoa kipaumbele na kukabiliana na changamoto ya unyanyapaa na Imani potofu dhidi ya wazee na uzee, na pia kuwawezesha wazee kutambua umuhimu wao katika kuwa na maisha bora ya kiutu na kuzingatia haki za binadamu.

Katika ujumbe wake kwa siku hii ambayo huadhimishwa Oktoba Mosi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema , wakati wazee hufurahia kupewa heshima fulani , ukweli ni kwamba katika jamii nyingi wazee wanatengwa na kutothaminiwa , hali ambhayo inawaathiri pakubwa.

Amesema kutokomeza unyanyapaa dhidi ya uzee na kutimiza haki za binadamu dhidi ya watu hao ni hulka na maadili bora, hivyo ametoa wito wa hatua kuchukuliwa kushughulikia ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wazee na kuwahakikishia usawa kisheria kuepusha sera za kibaguzi dhidi yao.

Kwa mujibu wa takwimu wazee wenye umri wa miaka 60 au zaidi ni takribani milioni 12.3 ya idadi ya watu wote duniani , na ifikapo mwaka 2050 idadi hiyo inatarajiwa kufikia milioni 22 limesema shirika la idadi ya watu duniani UNFPA

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter