Mustakhbali wa Burundi na DRC uko mikononi mwa jumuiya ya kimataifa:

30 Septemba 2016

Mustakhbali wa kijamii na kisiasa kwa mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Burundi kwenye ukanda wa maziwa makuu, uko mikononi mwa nchi husika na wadau wote wa ukanda mzima, Jumuiya ya Afrika Mashariki na jumuiya ya kimataifa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa mkutano wa kiamatifa kuhsu eneo la Maziwa Makuu, Zachary Muburi-Muita alipozungumza na idhaa ya Kiswahi ya Radio ya Umoja wa Mataifa.

Balozi Muita amesema upande wa serikali na upinzani katika mataifa hayo ni lazima kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya maslahi binafsi. Akianza na suala la Burundi Balozi Muita amemweleza Flora Nducha wa idhaa ya Kiswahili kwamba matumaini yapo lakini bado kuna changamoto

(MAHOJIANO NA MOBURI MUITA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter