Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 33 cha baraza la haki za binadamu chafunga pazia

Kikao cha 33 cha baraza la haki za binadamu chafunga pazia

Hatimaye leo Ijumaa kikao cha 33 cha baraza la haki za binadamu kimefunga pazia mjini Geneva Uswiss, kwa wito kwa nchi wanachama kuchukua hatua dhidi ya ukatili na uwajibikaji kwa wahusika.

Miongoni mwa maazimio yaliyopitishwa ni kura ya kuundwa kwa jopo la ngazi ya juu la uchunguzi nchini Burundi, kufuatia ripoti kwa baraza hilo ya machafuko yanayoendelea, yakihusishwa na uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kusalia muhula wa tatu madarakani.

Naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu Kate Gilmore,anasema chombo hicho kipo kwa ajili ya kutimiza matakwa ya nchi waanchama.

(SAUTI YA KATE GILMORE)

“Kila kitu unachotarajia kukiona kwa muktada wa misimamo mbalimbali kuhusu masuala kama vile watu wa asili, mwenendo wa kimapenzi, masuala ya wanawake,uhuru wa dini na kadhalika, mambo yote hayo yapo kwenye baraza na yanafanya kuwa muhimu sana , kuendelea kuwakumbusha na kuhakikisha nchi wanachama wanapata ushauri kuhusu viwango vya sheria za kimataifa zinavyosema ili tusijejikuta tunaingiza viwango ambavyo vinakinzana na sheria za kimataifa, hicho ni kitu cha muhimu sana kinachofanywa na ofisi yetu”

Mbali ya kupiga kura kwa maazimio zaidi ya 30 kwa nchi zinazokabiliwa na machafuko kama Jamhuri ya Kimokrasia ya Congo DRC, Sudan na Yemen, baraza hilo linajiandaa kuteua wachunguzi huru wapya watano wa haki za binadamu.