Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu launda kamisheni ya uchunguzi Burundi

Baraza la haki za binadamu launda kamisheni ya uchunguzi Burundi

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo wakati wa kikao chake huko Geneva, Uswisi, limepitisha azimio la kuunda kamisheni ya uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi.

Azimio hilo lililopitishwa kwa kura 19, huku saba zikipinga na 21 hazikuonyesha msimamo wowote linapatia kamisheni hiyo mamlaka ya mwaka mmoja ya kuchunguza ukiukwaji wa haki uliofanyika tangu mwezi Aprili mwaka 2015.

Halikadhalika kamisheni hiyo itawajibika kusaka watekelezaji wa ukiukwaji huo ili hatimaye waweze kuwajibishwa.

Burundi ambayo imepinga azimio hilo imesema ni masikitiko kuwa limepitishwa ikidai kuwa masuala mengi yaliyojumuishwa hayajakaguliwa na imeomba hatua zichukuliwe ili baraza la haki lisiwe la kisiasa.