Neno la Wiki - "Pete"
Wiki hii tunaangazia neno “PETE” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. pete lina zaidi ya maana moja, moja ikiwa ni pambo la ahadi linalovaliwa kwenye kidole, pili ni tundu kubwa kwenye sikio la mwanamke ili kutuliwa pambo la karatasi au la herini. Maana nyingine ni pambo lenyewe la karatasi linalotiwa kwenye matundu makubwa sikioni mwa mwanamke .