Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala Burundi na DRC ni mtihani, lakini tunaweza kushinda:Balozi Muita

Suala Burundi na DRC ni mtihani, lakini tunaweza kushinda:Balozi Muita

Hali ya kibinadamu na kisiasa katika nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ni changamoto na mtihani ambao viongozi wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki, eneo la maziwa makuu na Umoja wa Mataifa wanapaswa kukusanya nguvu pamoja kulipatia ufumbuzi.

Kauli hiyo imetolewa na balozi Zachary Muburi-Muita, Katibu Mkuu wa mkutano wa kimataifa wa Maziwa Makuu.

Akizungumza na idhaa hii amesema, Burundi hali ya usalama inaimarika na mchakato wa mazungumzo unaendelea Arusha,Tanzania, lakini hatima ya kisiasa bado iko njia panda

(SAUTI MUBURI- MUITA)

Na kwa upande wa DRC inayojiandaa na uchaguzi mwaka huu Bwana Muburi-Muita amesema..

(SAUTI MUBURI-MUITA)