Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumeshangazwa na mabadiliko ya ratiba ya uchaguzi Somalia: Baraza la Usalama

Tumeshangazwa na mabadiliko ya ratiba ya uchaguzi Somalia: Baraza la Usalama

Baraza la Usalama leo limetoa taarifa likieleza kusikitishwa na uamuzi wa kubadili ratiba ya uchaguzi nchini Somalia.

Tangazo hilo lilitolewa tarehe 26 mwezi huu na timu ya utekelezaji wa uchaguzi ya Somalia, (FIEIT), ambayo imesema mchakato wa uchaguzi nchini humo unahitaji muda zaidi.

Wanachama wa baraza hilo wametoa wito kwa wadau husika kufikia makubaliano kuhusu changamoto za kisiasa zilizosalia haraka iwezekanavyo, na kuheshimu na kuendeleza mchakato huo ndani ya ratiba hiyo mpya.

Vile vile baraza limesisitiza umuhimu wa uwepo wa mchakato wa uchaguzi wenye amani, wazi na jumuishi, kwani hayo yataweka misingi ya ki demokrasia na utulivu, misingi ambayo itaendeleza mafanikio yaliyopatikana hadi sasa nchini humo.