Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi Burundi inajumuisha wa awali kabla ya machafuko: Mbilinyi

Idadi ya wakimbizi Burundi inajumuisha wa awali kabla ya machafuko: Mbilinyi

Licha ya kuimarika kwa hali ya usalama, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Burundi limekiri kuwa idadi ya wakimbizi wanaosaka hifadhi nje ya taifa hilo imeongezeka lakini idadi hiyo inajumuisha wakimbizi waliokuwepo katika nchi hizo awali.

Katika mahojiano na idhaa hii Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini humo Abel Mbilinyi amefafanua kuwa idadi iliyotolewa mapema wiki hii na UNHCR ya laki tatu inatokana na ukweli kwamba.

(SAUTI MBILINYI)

Mbilinyi kadhalika amesema UNHCR ilikuwa na mkutano mapema wiki hii jijini Nairobi, Kenya kujadili hali ya wakimbizi na wahamiaji katika ukanda wa maziwa makuu.

(SAUTI MBILINYI)