Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kasi ya ukuaji uchumi Afrika; Rwanda, Tanzania na Ethiopia kidedea- Ripoti

Kasi ya ukuaji uchumi Afrika; Rwanda, Tanzania na Ethiopia kidedea- Ripoti

Mwelekeo wa ukuaji uchumi barani Afrika unatarajia kutwama zaidi na kuwa asilimia moja nukta sita mwaka huu ikilinganishwa na asilimia tatu mwaka jana, hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Benki ya dunia itolewayo mara mbili kwa mwaka, Africa’s Pulse. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

Ripoti hiyo inasema mwelekeo wa ukuaji unatofautiana ambapo baadhi ya nchi ukuaji unatwama huku nyingine uchumi unakua. Mathalani Rwanda, Tanzania na Ethiopia ukuaji wa uchumi kwa wastani ni zaidi ya asilimia sita kwa mwaka huku, Cote d’Ivoire na Senegal zikichomoza zaidi.

Mchumi mkuu wa Benki ya dunia kuhusu Afrika Albert Zeufack amesema chanzo cha kutwama uchumi ni kudorora kwa bei za bidhaa ikiwemo mafuta, hali ngumu ya kifedha na sera za uchumi zisizo makini.

Benki ya dunia inasema mwelekeo ni kupanua wigo wa bidhaa zinazouzwa pamoja na kuboresha sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo ili kuinua vipato vyao na kupunguza umaskini.