Skip to main content

Unyanyapaa dhidi ya uzee unabana fursa na kufupisha maisha:WHO

Unyanyapaa dhidi ya uzee unabana fursa na kufupisha maisha:WHO

Uzee hukabiliwa na aina kubwa ya unyanyapaa na ubaguzi ambao una madhara mabaya kwa afya ya mtu, kama ilivyo kwa ubaguzi wa rangi na jinsia.

Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni, WHO, uzee uko kila mahali, katika utamaduni maarufu, katika lugha, na sera kama vile umri wa lazima kustaafu. Mitazamo hii na mazoea huwatenga watu wazima na inaongoza kwa kuwaengua katika jamii.

Utafiti unaonyesha kwamba mitazamo hasi dhidi ya uzee inaweza hata kufupisha maisha ya mtu kwa miaka 7.5. Dr John Beard ni mkurugenzi wa WHO idara ya maisha na uzee

(SAUTI YA DR JOHN BEARD)

Kuna ushahidi mzuri kwamba, watu wenye mawazo hasi wakati wanapozeeka ina athari nyingi hata kupunguza maisha yao, kuliko watu wenye mitazamo chanya”

Katika kuadhimisha siku ya wazee duniani, ambayo hufanyika Oktoba Mosi, WHO imeandaa kampeni maalumu itakayoendeshwa kwenye mtandao iitwayo “Chukua msimamo dhidi ya ubaguzi wa uzee”