Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rushwa Tanzania ilishapevuka, sasa tunachukua hatua- Tanzania

Rushwa Tanzania ilishapevuka, sasa tunachukua hatua- Tanzania

Jumatatu ya Septemba 26, Tanzania iliwasilisha hotuba yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakati wa kikao cha mjadala mkuu wa wazi ambao hufanyika kila Septemba, mkutano wa baraza hilo unapoanza rasmi. Dkt. Augustine Mahiga ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki aliwasilisha hotuba iliyogusa masuala ya yanayogusa misingi ya Umoja wa Mataifa ambayo ni amani, usalama, maendeleo na haki za binadamu. Punde baada ya kuhutubia, Balozi Mahiga alihojiwa na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa ambapo ameelezea hatua za kudhibiti rushwa, kuendeleza vijana na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini hapa anaanza kwa kuelezea ujumbe wake kutoka kwa Rais John Magufuli.