Dhamira ya dunia ni muhimu kwa mustakhbali wa Afghanistan: Tadamichi Yamamoto

28 Septemba 2016

Ushirika baina ya Umoja wa Mataifa na Afghanistan umeanza kitambo , tangu 1946 ambapo nchi hiyo ilijiunga kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Miongo kadhaa baadaye baada ya kuangaka kwa utawala wa Taliban, na kuanzishwa kwa serikali ya mpito , baraza la usalama likaanzisha mpango wa usaidizi nchini humo ujulkanao kama UNAMA.

Mwakilishi maalumu wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini, UNAMA, Tadamichi Yamamoto, amerzungumza na Umoja wa Mataifa kabla ya kuelekea kwenye mkutano kuhusu Afghanistan hapo Oktoba 4 na 5.

Masuala aliyozungumzia na kazi za Umoja wa Mataifa , katika nchi hiyo ya Asia ya Kati na changamoto inazokabiliana nazo katika mchakato wa kuelekea amani ya kudumu.

Yamamoto ameelezea msaada na dhamiya ya jumuiya ya kimataifa kwa taifa hilo kuwa ni wa muhimu kwa mchakato wa mustakhbali wa nchi hiyo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter