Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya haki za binadamu CAR watishiwa na ugaidi- mtaalamu

Hali ya haki za binadamu CAR watishiwa na ugaidi- mtaalamu

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati,  Marie-Therese Keita Bocoum leo amewasilisha ripoti yake mbele ya baraza la haki la Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi kuhusu hali ya haki za binadamu nchin  humo CAR. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Katika taarifa yake ya tatu mbele ya baraza hilo, Bi Keita-Boucoum amesema ugaidi unaofanywa na vikundi vilivyojihami nchini humo vinaendelea kukandamiza haki za wananchi licha ya kuwepo kwa serikali iliyochaguliwa na umma.

Ametaka serikali za mitaa kuchagiza mazungumzo baina ya wananchi katika jamii zao ili watoe shaka na shuku zao na kwa upande wa serikali..

(Sauti ya Marie)

“Natoa wito kwa serikali kuendelea na mazungumzo na vikundi hivyo ili kupata mkataba wa kuanzisha mpango wa vikundi hivyo kujisalimisha, kupokonywa silaha na kujumuishwa kwenye jamii.”