Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD yataka nchi zipendekeze majina ya Rais atakayesongesha SDGs

IFAD yataka nchi zipendekeze majina ya Rais atakayesongesha SDGs

Shirika la kimataifa la ufadhili wa maendeleo ya kilimo (IFAD) kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya fedha leo hii wametangaza kwa nchi wanachama kupendekeza majina ya mgombea wa Urais wa shirika hilo.

Hii ni nafsi ya juu zaidi kwa IFAD, ikiwa na jukumu la kuongoza shirika na bodi kuu.

Taarifa ya IFAD imezitaka nchi wanachama kuwasilisha majina ya wateule wao kwa Katibu kabla ya Desemba mosi huku ikisisitiza kuwa Rais ajaye atakuwa na jukumu na kipaumbele cha mipango ya maendeo endelevu SDG, hususani katika kukomesha njaa.

Mabadiliko ya tabia nchi na uhifadhi wa mazingira hususani katika nchi zinazoendelea yametajwa na shirika hilo kama ni kipuambele muhimu wakati huu.

Rais wa IFAD atateuliwa na mkutano mkuu wakati wa kikao chake mnamo 14 Februari mwakani jijini Roma,Italia.