Skip to main content

Hali ya haki za binadamu Burundi ni mbaya-Tume

Hali ya haki za binadamu Burundi ni mbaya-Tume

Tume huru ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi nchini Burundi leo imewasilisha ripoti yake ya mwisho mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo huko Geneva, Uswisi.

Tume hiyo iliyojumuisha wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika ilipewa mamlaka ya kuchunguza ukiukwaji wa haki za biandamu nchini Burundi na kutoa mapendekezo juu ya uboreshaji wa haki hizo na msaada wa kiufundi katika maridhiano na utekelezaji wa mkataba wa Arusha. Rosemary Musumba na taarifa zaidi.

(Taarifa ya RoseMary)

Kiongozi wa tume hiyo Christof Heyns amesema wamebaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa na serikali.

Amesema hakuna uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa habari na wamebaini hofu kubwa miongoni mwa wananchi na hata wale wa jirani, akisema hilo litafuatiliwa kwa karibu, na akaongeza...

(Sauti ya Heyns)

"Serikali imeaonyesha nia ndogo au nia ya kuzuia au kukomesha ukiukwaji huu mkubwa. Tangu kuanza kwa mgogoro, hakuna uwajibikaji kutoka kwa vikosi vya usalama au kundi cha chama tawala cha Imbonerakure"

Halikadhalika amesema hali inazidi kuwa mbaya na majukumu ya kutatua tatizo hili lipo kwa serikali ya Burundi, Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika.