Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Al Mahdi afungwa miaka tisa jela kwa uharibifu wa mali za kitamaduni Mali

Al Mahdi afungwa miaka tisa jela kwa uharibifu wa mali za kitamaduni Mali

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, imetambua  hatia ya Ahmed Al-Faqi Al-Mahdi ya uhalifu wa kivita na imemuhukumu miaka 9 jela kwa wajibu wake katika uharibifu wa makusudi  wa makavazi tisa na lango la siri la msikiti wa Sidi Yahia mwaka 2012 .

Maeneo hayo yako urithi wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO mjini Timbuktu Mali.

Jaji Raul Cano Pangalangan ndiye alisoma hukumu ya Al-Mahdi.

(Sauti ya Jaji Raul)

“Mahakama kwa kauli moja inakuhukumu miaka tisa jela. Kwa mujibu wa kanuni za rufaa, muda uliokuwepo rumande tangu ukamatwe tarehe 18 Septemba mwaka 2015 utapunguzwa kwenye hukumu yako.”

Akizungumzia hukumu hiyo mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema..

(Sauti ya Irina)

“Naweza kusema hili ni jambo muhimu sana. Inamaanisha ukwepaji sheria hauwezi kuruhusiwa. Huu ni uhalifu na lazima washtakiwe kisheria. Kama tunasema tuna sheria ya kimataifa, tuna kanuni, basi tuwepo hapo kama inavyotarajiwa.”