Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo la viongozi wa dunia 29 kushika bango utapiamlo, Kikwete mmojawao

Jopo la viongozi wa dunia 29 kushika bango utapiamlo, Kikwete mmojawao

Vuguvugu la kuchagiza lishe (SUN) linaendelea na shughuli ya kupigia upatu lishe bora kwa wote, kila mahali , hasa sasa ambapo viongozi wa dunia 29 walioteluiwa wataongeza nguvu ya vita dhidi ya aina zote za utapia mlo.

Viongozi hao walioteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, ni vinara wal;ioahidi kuwaka suala la lishe kama kitovu cha ajenda yao , na kuchagiza na kutoa muongozo kwa vuguvugu la SUN na nia yake yay a kutokomeza utapia mlo.

Takwimu za kimataifa zinaonyesha kwamba mtu mmoja kati ya watatu anaugua utapia mlo duniani , na wavulana na wasicha takribani milioni 156 kote duniani wana matatizo ya kudumaa.

Akizungumzia tatizo hilo Ban amesema “lishe bora ni muhimu sana katika kufikia ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, na kusema kuna fursa sasa ya kufanya kazi pamoja kubadilisha hali hiyo.”

Kundi hilo la viongozi 29 wasaidia juhudi za nchi mbalimbali za kusukuma mchakato wa lishe na kutimiza malengo kwa wavulana, wasichana na familia zao ili kuwe na dunia huru bila utapia mlo ifikapo 2030.

Miongoni mwa viongozi hao walioteuliwa ni Rais wa Guatemala, Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu SDG’s, Bwana David Nabarro, Jakaya Kikwete Rais wa zamani wa Tanzania, na Bwana Akin Adesina Rais wa bank ya maendeleo ya Afrika.