Skip to main content

Dunia inakabiliwa na tishio kubwa la nyuklia:Eliasson

Dunia inakabiliwa na tishio kubwa la nyuklia:Eliasson

Dunia inakabiliwa na tishio kubwa la ongezeko la nyuklia, na juhudi za mchakato wa upokonyaji silaha hizo umegonga kisiki, amesema naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Jan Eliasson ameyasema hayo Jumatatu wakati wa mkutano wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya utokomezaji wa silaha za nyuklia. Hafla hiyo imeandaliwa kandoni mwa mjadala wa baraza kuu la 71.

Mamilioni ya dola zimetengwa kuhakikisha utunzaji na ukarabati wa mfumo ambao tayari ni mkubwa wa sialaha za nyuklia, ameonya bwana Eliasson.

Ametolea mfanyo Korea ya Kaskazini ambayo tayari imekiuka mara kadhaa sheria za majaribio ya nyuklia na natajkwa ya jumuiya ya kimataifa.

Ameongeza kuwa kwa bahati mbaya nchi nyingi zinaendelea kujumuisha nyuklia katika nyaraka zao za usalama.

(SAUTI ELIASSON)

"Lakini hebu tukumbuke kwamba maendeleo ya hivi karibuni yanaonyesha kwamba silaha za nyuklia , hazituhakikishii amani na usalama. Badala yake utengenezaji na umiliki wake umekuwa ni chanzo kikubwa cha ongezeko la mivutano. Na wakati huohuo tunashuhudia mgawanyiko mkubwa dhidi ya mustakhbali wa upokonyaji wa silaha za nyuklia. Tathimini ya mzunguko mwingine wa mkataba wa kupinga matumizi ya sialaha za nyuklia (NTP) utaanza 2017. Dunia haiwezi kumudu kipindi kingine cha hatari ya kutochukua hatua.”