Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan panua wigo wa vyanzo vya mapato ya kiuchumi- Ripoti

Sudan panua wigo wa vyanzo vya mapato ya kiuchumi- Ripoti

Ripoti mpya ya benki ya dunia kuhusu uchumi wa Sudan imeitaka nchi hiyo kusaka mbinu za kupanua wigo wa vyanzo vyake vya kiuchumi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uchumi wa Sudan umesinyaa baada ya Sudan Kusini kujtenga mwaka 2011 na kupoteza asilimia 75 ya mapato yake yaliyokuwa yakitokana na mafuta.

Kwa sasa Sudan imesaka vyanzo vipya ikiwemo kuuza nje dhahabu na mifugo lakini benki ya dunia imetaka nchi hiyo pamoja na vyanzo hivyo ifanye marekebisho ya kimuundo na sera za uchumi mkubwa ili ukuaji wa kiuchumi uweze kuwa dhahiri.

Mwandishi kiongozi wa ripoti hiyo Michael Geiger amesema pamoja an marekebisho hayo, Sudan ichukue hatua idhibiti mfumuko wa bei na iongeze tija kwenye kilimo.