Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira bora ya kazi, yaimarisha malipo na ufanisi viwandani:ILO

Mazingira bora ya kazi, yaimarisha malipo na ufanisi viwandani:ILO

Uboreshaji wa mazingira ya kazi katika viwanda vya nguo ambayo kawaida huwa na malipo dunia , hakuathiri uzalishaji au faida , umesema Umoja wa Mataifa Jumatatu.

Kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO mamia ya viwanda katika nchi saba zinazoendelea vimeshuhudia uboreshaji mkubwa shukrani kwa mpango wa kazi bora.

Mpango huo unajumuisha mishahara mikubwa na uzalishaji, sanjari na upunguzaji wa vitendo vya unyanyasaji na kutumia nguvu. Mchumi Drusilla Brown ni kutoka chuo kikuu Tufts hapa Marekani.

(SAUTI YA DRUSILLA BROWN)

"Kama ukiangalia kipimo cha malipo ya kila wiki kwa dola za Marekani tunaona ongezeko la dola saba kwa wiki baada ya miaka mitatu cha mfiduo, je Kazi bora kupunguza saa? jibu la swali hilo ni ndiyo, tunaona punguzo la saa 3.5 baada ya kuwa katika mpango."

Mpango huo ulianzishwa mwaka 2009 na ILO kwa ushirika na Bank ya dunia na unaangalia viwanda 1300 vye nye wafanyakazi zaidi ya milioni 1.6 katika nchi saba zikiwemio Bangladesh,Vietnam, Indonesia , Jordan na Haiti.