Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twataka mazungumzo yatakayoheshimu katiba- Burundi

Twataka mazungumzo yatakayoheshimu katiba- Burundi

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Alain Nyamitwe, leo amekiri umuhimu wa mazungumzo baina ya wadau Burundi endapo tu yataheshimu katiba  ya nchi hiyo.
Bwana Alain amesema hayo wakati wa hotuba yake kwenye kikao cha 71 cha Baraza Kuu.
Kuhusu migogoro ya hivi karibuni, amesema wananchi wametoa wito wa mabadiliko muhimu yanayohitajika kuleta amani, katika ripoti ya iliyotolewa na tume ya uchunguzi, wito ambao serikali ya Burundi umeusikia na utazingatia.
Pia amesisitiza kuwa serikali yake inahakikisha usalama wa raia wote na kuimarisha haki za binadamu, bila kujali kabila, huku akisisitiza kuwa ni lazima tathmini zozote zinazohusu haki za binadamu nchini Burundi zitekelezwe kwa tahadhari kuepuka taswira hasi kwa taifa.
Na kuhusu malengo ya maendeleo endelevu.
( SAUTI NYAMITWE)
 ''Burundi imejizatiti  kuwaweka wananchi wake katika muelekeo wa sera ya maendeleo, kwa msaada wa wadau, serikali ya Burundi itasaidia mahitaji ya walio katika hali hatarishi.''