Skip to main content

Ban, UNICEF walaani shambulio la anga Allepo.

Ban, UNICEF walaani shambulio la anga Allepo.

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la anga  mjini Allepo nchini Syria hapo jana linalotajwa kuharibu miundo mbinu muhimu.

Taarifa ya msemaji wa Ban iliyotolewa leo Jumamosi, imesema Ban ameitaka jumuiya ya kimataifa kungana kupinga matumizi holela ya silaha nchini humo katika maeneo ya raia.

Katika hatua nyingine Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limelaani shambulio mjini Allepo nchini Syria lilisoababisha kukatika kwa huduma ya maji na hivyo kuathiri zaidi ya watu laki mbili na nusu.

Machafuko yanazuia timu za matengenezo kuyafikia maneo husika,  imeongeza UNICEF katika taarifa yake na kusema kuwa shambulio liliharibu kituo cha pampu za maji cha Bab al Nayrab na kama hilo halitoshi upande mwingine kinzani katika machafuko umelipiza kwa kukata pampu za maji katika kituo kiitwacho Suleiman al Halabi

Shirika hilo limesema kuwa hali hiyo tete inawaweka watoto katika hatari ya kuuugua magonjwa ya milipuko  na kuongeza madhila na hofu ambayo watoto wamekuwa wakipitia kila siku huko Allepo.

UNICEF kadhalika imesema kuwa jamii za Mashariki mwa Allepo zitalazimika kutumia maji  yaliharibiwa  wakati kwa upande wa Magharibi visima vya maji vitatoa majai salama kama mbadala.