Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM, na wadau walaani vurugu DRC.

UM, na wadau walaani vurugu DRC.

 

Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika AU, muungano wa ulaya EU, na shirika la kimataifa la nchi zinazozungumza kifaransa IOF, wameelezea kusikitishwa kwao na machafuko ya hivi kribuni mjini Kinshasa na maeno mengine nchini Jamhuri ya Kidemokaria ya Congo DRC  yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa.

Taarifa ya pamoja ya vyombo hivyo imetaka wadau wa kisiasa,  wakiwamo mamlaka ya Rais na upinzani kujizuia kwa vitendo na matamshi na kuwasihi wafuasi wa vyama vyao,  kujizuia dhidi ya machafuko.

Wamezitaka mamlaka za DRC kukuza na kulinda haki za binadamu na uhuru wa kimsingi kwa mujibu wa katiba hasa pale wanapokuwa wanatekeleza amri kwa uma.

Taarifa hiyo pia inasisitiza kuwa wadau wote wakiwemo maafisa wa sheria na usalama wana wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia utawala wa kisheria na haki za binadamu na wakishindwa kufanya hivyo watawajibishwa.