Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama umerejea Sudan Kusini, tunaimarisha uchumi sasa: Gai

Usalama umerejea Sudan Kusini, tunaimarisha uchumi sasa: Gai

Naweza kuwahakikishia kuwa sasa taifa langu lina utulivu na maisha sasa yamerudi katika hali ya kawaida, ni kauli ya Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Taban Deng Gai wakati akilihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika mkutano wake wa 71 unaoendelea mjini New York.

Hata hivyo makamu huyo wa Rais aliyeteuliwa hivi karibuni amekirikuwa machafuko yaliyoibuka miezi ya hivi karibuni yamezorotesha uchumi kwa kiwango kikubwa na kusema kile ambacho kinafanyika kwa sasa.

(SAUTI GAI)

‘‘Tunafanya kila tuwezalo kushughulikia mitikisiko hii ya kiuchumi kupitia uhilimivu wa kiusalama, kuimarisha sera za fedha, kuimarisha kipato kitokanacho na mafuta, kujihusisha na shughuli za kilimo, madini, utalii ikiwa ni pamoja utalii wa mazingira na kuhamasisha watalii kuja Sudan Kusini.’’

Bwana Gai amesema kwamba utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs unatekelezwa kwa ubia na nchi kama vile Kenya ,Uganda na Ethiopia kwa kuhakikisha kwamba huku kipaumbele kikiwa ni ujenzi wa miundo msingi kam vile barbara na nishati ili kuinua kiwango cha maisha ya raia.