Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhila ya wakimbizi na usadizi kwa kundi hilo

Madhila ya wakimbizi na usadizi kwa kundi hilo

Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamekutana mjini New York nchini Marekani  juma hili kuangazia  maswala ya wakimbizi na wahamiaji. Imedhihirika wazi kuwa msaada kwa wakimbizi umekuwa unapungua siku hadi siku.

Wakiratibiwa na wadau wa mashirika ya misaadaya kibinadamu kama ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, shirika la Umoja wa Mataifa lakuhudumia wakimbizi UNHCR na wengineo, wameihimiza jumuiya ya kimataifa kuchangia ili kustawisha wakimbizi walioko katika nchi zinazoendelea

Akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa usaidizi wa wakimbzi na wahamiaji ikiwa ni sehemu ya mijadala ya kikao cha 71 cha baraza kuu la UM,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa viongozi wa dunia , asasi za kiraia na mashirika ya kimataifa kusongesha mbele hatua kubwa za mabadiliko ili kushughulikia ongezeko kubwa na athari za migogoro ya kibinadamu inayosababisha ukimbizi.

Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Maziwa Makuu barani Afrika huko Jamhuri ya Kidemokraia ya Kongo DRC na hata Burundi.

Katika kufahamu hali ya wakimbizi, mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA ametembelea kambi ya Kavumu ikiwa ni moja ya kambi za wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokaria ya Congo ilioko mashariki mwa Burundi katika mkoa wa Cankuzo na kutuandalia makala ifuatayo.