Skip to main content

CAR imezipa kisogo siku za kiza na machafuko:Rais Touadera

CAR imezipa kisogo siku za kiza na machafuko:Rais Touadera

Akihutubia katika mjadala wa wazi wa baraza kuu la Umoja wa mataifa Rais Faustin Archange Touadera, wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), ameushukuru Umoja wa Mataifa na jumuiya nzima ya kimataifa kwa kulisaidia taifa hilo kurejea katika hali ya utulivu na utawala wa sheria.

Kupitia sauti ya mkalimani amesema ameweka mikakati kuhakikisha kasi ya kusaka amani ya kudumua inaendelea

(TOUADERA CUT 1)

“Jamhuri ya Africa ya Kati imezipa kisogo siku za kiza.Tunashirikiana pamoja kuijenga upya nchi yetu kwa kufanya mabadiliko yanayohitajika”

Ameongeza kuwa tangu alipoingia madarakani amefanya mabadiliko mengi katika taasisis za serikali ikiwemo kupambana na ufisadi na kushughulikia suala la ukwepaji sheria, lakini bado kuna kibarua.

(SAUTI YA TOUADERA 2)

“Jamhuri ya Afrika ya Kati ni kweli imerejea katika demokrasia lakini hali bado ni tete, nab ado kuna kazi kubwa ya kufanya”

Ameongeza kuwa nia yake ni kuileta nchi nzima pamoja ili kudumisha amani na usalama, upatanisho wa kitaifa, kufufua uchumi, haki na haki za binadamu.