Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi wa Burundi yavuka 300,000

Idadi ya wakimbizi wa Burundi yavuka 300,000

Ikiwa ni miezi kumi na nane tangu kuibuka kwa mzozo wa kisiasa nchini Burundi, Aprili 2015, watu zaidi ya laki tatu wamekimbilia nchi jirani ikiwemo Tanzania, Uganda na Rwanda wakisaka usalama. John Kibego na taarifa kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbimzi, UNHCR, wengi wao wamekimbia mikoa ya Muyinga, Makamba, Cankuzo, Kirundo an Ruyigi wakisaka aidah hifadhi ama ulinzi wa kimataifa.

Imesema mwaka huu imeshuhudia ongezoko la wakimbizi ambapo zadi ya 20,000 walikimbia mnamo Julai na Agosti kufuatia vurugu, mauaji, vitisho, utekajinyara na metoso.

Kufuatia hali hiyo, UNHCR, inaomba jamii ya kimataifa kuendeleza juhudi za kurejesha amani Burundi na kuongeza msaada wa kiutu katika nchi zinazowahifadhi ili kuwezesha upatuikanaji wa mahitaji ya msingi, elimu, afyaKufua na wakimbizi hao kujikimu.