Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchakato wa amani Sudan Kusini wajadiliwa UM

Mchakato wa amani Sudan Kusini wajadiliwa UM

Masuala ya mchakato wa amani wa Sudan Kusini leo, yanaangaziwa katika kikao cha mawaziri kandoni mwa mjadala wa baraza kuu  cha 71 kwenye Umoja wa Mataifa.

Naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataongoza mkutano huo, unaohudhuriwa na wakilishi wa Sudan kusini, Uchina, Umoja wa Afrika, Kamisheni ya pamoja ya kufuatilia na kutathmini hali nchini Sudan Kusini, JMEC,  mkuu wa opreseshni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous na shirika la kiserikali la maendeleo pembe ya Afrika IGAD,

Akizungumza na idhaa hii kabla ya kuanza kwa kikao hicho  katibu mtendaji wa shirika la IGAD, Balozi Mahboub Maalim amefafanua nia yao..

(Sauti ya Balozi Maalim)