Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yatiwa hofu na kuzidi kuzorota kwa hali Yemen

Ofisi ya haki za binadamu yatiwa hofu na kuzidi kuzorota kwa hali Yemen

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa wasiwasi na ongezeko la athari za machafuko kwa raia nchini Yemen, huku mazungumzo ya amani yakisitishwa kwa muda.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo watu 180 wameuawa na wengine 268 kujeruhiwa mwezi Agosti pekee, ikiwa ni ongezeko la asilimia 40 ikilinganisha na mwezi wa Julai. Cecile Pouilly ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva

(SAUTI YA CECILE POUILLY)

“Kumekuwa na ongezeko la idadi ya mashambulizi dhidi ya vitu vya raia vinavyolindwa, takribani matukio 41 yametokea na kuathiri majengo ya elimu na afya, masoko, nyumba za ibada, viwanja vya ndege na nyumba za raia kwa mwezi Agosti.”

Ameongeza kuwa hofu yao kubwa ni eneo la Taizz ambnako vikwazo vilivyowekwa na kamati zinazohusiaka na Houthi zimesababisha upungufu wa bidhaa muhimu kama chakula, maji, mafuta ya na kutaka kusambaratisha kabisa mfumo wa afya.