Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msichana mwenye ndoto ni moto: Rebecca

Msichana mwenye ndoto ni moto: Rebecca

‘‘Msichana mwenye ndoto ni moto, hakamatiki.’’ ni kauli ya mshindi wa tuzo ya UNICEF inayotambua juhudi za kuokomeza ndoa za utotoni nchini Tanzania, Rebeca Gyumi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali liitwalo Msichana.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii mjini New York, Rebecca amesema taifa linapaswa kutambua kuwa harakati za maendeleo hazitafanikiwa ikiwa kundi la wasichana halitapewa kipaumbele hususani katika kuhakikisha wanaondokana na changamoto ya ndoa za utotoni.

Kwanza anaanza kueleza shirika analoliongoza linafanya nini nchini humo katika kuwakwamua wasichana dhidi ya ndoa za utotoni.