Vita, mizozo na ugaidi sasa vimezoeleka- Holy See
Kuendelea kwa muda mrefu kwa vita na mizozo duniani bila kupatiwa ufumbuzi wowote kunaashiria pengine ulimwenguni umekubali mwelekeo huo kuwa hali ya kawaida.
Ni kauli ya Muadhama Pietro Kardinali Parolin aliyotoa wakati akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo akiwakilisha Holy See.
Ametaja mizozo huko Maziwa Makuu, Sudan Kusini bila kusahau mashariki mwa Ukraine akisema..
(Sauti ya Kardinali Parolin)
“Ijapokuwa hali mbaya katika nchi hizo zimeendelea kwa muda mrefu na kusababisha machungu makubwa kwa binadamu, bado tuko mbali sana kupata suluhu na inaonekana kuwa tumekubali mizozo, vita na ugaidi kuwa hali ya kawaida ya maisha.”
Kardinali Parolin amesema pamoja na kusaka uharaka wa kusitisha mapigano, kuheshimu utu na haki za watu na kuwasilisha misaada ya kibinadamu..
(Sauti ya Kardinali Parolin)
“Kuna umuhimu pia wa kuwezesha mashauriano na wale wanaowajibika moja kwa moja au kwa njia nyingine na mzozo.”