Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na Tanzania wasajili watoto wa chini ya miaka 5 na kuwapa vyeti vya kuzaliwa

UNICEF na Tanzania wasajili watoto wa chini ya miaka 5 na kuwapa vyeti vya kuzaliwa

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto nchini Tanzania UNICEF na serikali ya nchi hiyo wamezindua hatua mpya ya usajili wa watoto wote wanaozaliwa na walio na umri wa chini ya miaka mitano. Mradi huo ulioanza mwaka 2012 kwa majaribio una lengo la kufikia mikoa yote ya Tanzania.

Hadi sasa watoto 400,000 wameshasajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa katika mikoa ya Mbeya na Mwanza. Na safari hii kampeni imeingia mikoa ya Iringa na Njombe. Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo waziri wa mambo ya katiba na sheria wa Tanzania Dr Harrison Mwakyembe amesema..

(SAUTI YA MWAKYEMBE)

Naye mwakilishi wa UNICEF Tanzania Maniza Zaman akihimiza umuhimu wa usajili huo amesema..

(SAUTI YA MANIZA)

"Naamini juhudi kama hizi zitafika mbali katika kuwa na usajili bora na mfumo muhimu wa takwimu katika nchi hii. Uzinduzi wa leo unafungua hatua mpya ya kurahisisha usajili wa vizazi na kwa gharama nafuu kwa watoto wote Tanzania"

Tanzania ina kiwango kidogo cha usajili wa watoto wanapozaliwa , na hii inamaanisha kwamba mamilioni ya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano hawatambuliki.