Ripoti yazinduliwa kuchochea wanawake kiuchumi

22 Septemba 2016

Harakati za kuwezesha wanawake kiuchumi zimepigiwa chepuo hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati wa kikao cha jopo la ngazi ya juu lililopatiwa jukumu la kutafiti na kuibuka na ripoti. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

Nats..

 Video maalum ya kuonyesha harakati za kiuchumi za wanawake dunia iliporomoshwa mwanzo wa kikao, cha  ripoti hiyo iliyoandaliwa na jopo hilo la zaidi ya watu 10.

Ripoti hiyo ya kwanza kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa imetaja mambo saba ya kuchochea kuchipua kwa wanawake kiuchumi ikiwemo kazi zinazofanywa na wanawake bila ujira.

Winnie Byanyima ni mmoja wa wajumbe wa jopo hilo.

(Sauti ya Winnie)

"Tunaangalia vikwazo vya kimfumo badala ya kutibu dalili pekee. Ripoti hii inalenga kufanya hivyo. Kimsingi kazi ya jopo hili haiwezi kufumbia macho uchumi ambao unaengua makusudi wanawake na maskini, uchumi ambao unashindwa kuthamini kazi ya wanawake.”

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud