Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nilichokishuhudia kimenipeleka kuokoa maisha ya wahamiaji na wakimbizi

Nilichokishuhudia kimenipeleka kuokoa maisha ya wahamiaji na wakimbizi

Mimi na familia yangu tuliguswa sana na majanga yanayotokea katika pwani ya mediterenia na ndipo tukaamua kuchangia katika kuokoa maisha. Hayo ni maneno ya Christopher Catrambone, Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali linalokoa wahamiaji katika bahari ya mediterenia(MOAS).Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Christopher na familia yake kwa miaka miwili sasa wameokoa maisha ya zaidi ya wahamiaji 27,000, kupitia shirika lao lisilo la kiserikali, ambapo ameieleza Radio ya Umoja wa Mataifa kilichomsukuma kuanza kazi hii.

(Sauti ya Christopher)

"Nafikiri kuona na kushuhudia pande mbili hizi- na ni wazo ambalo hatujawahi kulifikiri- tukiwa likizoni ndani ya meli ya anasa, tulitambua na kujiuliza kuwa, sehemu hii ambayo sisi tunaifurahia , watu wanapoteza maisha yao".

Amesema chuki dhidi ya wahamiaji na wakimbizi itatokomea endapo kila mkazi wa dunia atajihusisha nao kwa karibu zaidi, ili kupata uelewa wa maisha halisi ya kundi hili.