Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WB, ILO watangaza mkakati kutoa ulinzi wa kijamii

WB, ILO watangaza mkakati kutoa ulinzi wa kijamii

Benki ya dunia WB, kwa kushirikiana na shirika la kazi ulimwenguni ILO, wanatekeleza mkakati wa kuyafikia makundi masikini na hatarishi katika kuyapatia ulinzi wa kijamii.

Kupitia mkakati uliopewa jina ubia wa kimataifa kwa ajili ya ulinzi uliotangazwa wakati wa mijadala ya kikao cha 71 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa , viongozi wameadhimia kuhakikisha hakuna watu wanokosa usaidizi wanapohitaji.

Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim amesema ulinzi wa kijamii unamaanisha kupunguza umasikini, kutekeleza usawa wa kijinisia,kupunguza ukosefu wa usawa wa kiuchumi na upatikanaji wa ajira.

Amesema wakati nchi nyingi zilizoendelea zimefanikisha makakati wa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma, takwimu katika nchi zenye kipato kidogo zinaonyesha kuwa ni mtu mmoja kati ya watu watano masikini na uhakika wa ulinzi wa kijamii.

Kwa upande wake Mkurugeni Mkuu wa ILO Guy Ryder amesema lengo la pamoja ni kuongeza idadi ya nchi zinazotoa ulinzi wa kijamii kubuni na kutekeleza mifumo ya ulinzi wa kijamii wa kimataifa.