Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwenye mkutano wa ngazi ya juu hapa katika Umoja wa Mataifa juu ya nchi ya Somalia hii leo

Kwenye mkutano wa ngazi ya juu hapa katika Umoja wa Mataifa juu ya nchi ya Somalia hii leo

Naibu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson, amezishukuru serikali za Ethiopia, Italia, Uingereza na Somalia kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huu kwa wakati muafaka, akisema ushiriki wao unaonyesha nguvu na msaada wa pamoja kwa ajili ya Somalia ya sasa na ya siku zijazo.

Akizungumza katika mjadala maalumu kuhusu Somalia kwenye Umoja wa mataifa hii leo, amesema anatambua mchango wa Muungano wa Afrika, nchi Wanachama kwa kuchangia askari wa kulinda amani wa AMISOM, washirika ikiwa ni pamoja na Muungano wa Ulaya, IGAD, Uturuki na mataifa ya Ghuba.

Bwana Eliasson ameipongeza serikali na watu wa Somaliakwa jukumu kubwa na kubuni njia mpya za kujiendeleza kwa nchi ambayo imeghubikwa na migogoro, umaskini, matatizo ya haki za binadamu na utawala wa sheria. Hasa wakati huu ambapo wanajiandaa na kupanga uchaguzi wa wabunge na Rais ikiwa na dhamira ya kuhifadhi moja katika viti vitatu katika bunge jipya kwa wanawake.

Ameutaja utaratibu huu wa uchaguzi kama hatua kubwa na kuwasihi wadau wote kuwajibika na kuratibu kwa haraka iwekezanavyo mchakato wa amani nakukubali matokeo. Ameongeza kuwa ushiriki wa Wasomali wote katika mchakato huu ni muhimu, kuleta usalama na mafanikio kwa maendeleo endelevu si tu kwa watu wa Somalia lakini pia kwa Afrika na jumuiya nzima ya kimataifa.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson akizungumzia uchaguzi huo wa Somalia amesema, mchango wao wa zaidi ya paundi milioni 7 kwa AMISOM, umeleta matumaini makubwa tayari kwa hatua nchi ya Somalia iliyofikia kimaendeleo lakini bado kuna kazi ya kufanya. Wengine waliohudhuria mkutano huo ni Michael Keating, mwakilishi wa Katibu mkuu nchini Somalia.