Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo ndio mpango mzima, vijana tusimame kidete: Rita

Kilimo ndio mpango mzima, vijana tusimame kidete: Rita

Akiwa na Umri wa miaka 25, Rita Kimani ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya FarmDrive nchini Kenya inayosaidia kuunganisha wakulima wadogo wadogo na fursa ya mikopo bila kuhitaji dhamana.

Kwa sasa kampuni hiyo yenye mwaka mmoja na nusu inasaidia wakulima zaidi ya Elfu Tatu. Jitihada hizi za Rita zimewezesha yeye kutangazwa mmoja wa viongozi vijana wa Umoja wa Mataifa wanaosongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Je Rita anafanya nini? Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza na Rita ambaye alitembelea Umoja wa Mataifa kutangazwa rasmi, na hapa anaanza kwa kuelezea kile wanachofanya.

(MAHOJIANO NA RITA)