Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto waepushwe na hatari ya kemikali na uchafuzi wa mazingira tangu utotoni :UM

Watoto waepushwe na hatari ya kemikali na uchafuzi wa mazingira tangu utotoni :UM

Hatari ya kuwepo kwenye chemikali zenye sumu na uchaguzi wa mazingira tangu utotoni ni hali inayochangia tatizo la kimyakimya ya maradhi ya utotoni na ulemavu ambao unapaswa kushughulikiwa katika ngazi ya kimataifa.

Hayo ni kwa mujibu wa mchunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa, akionya nchi wanachama wa Umoja huo na makampuni ya biashara.

Onyo hilo la mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa Baskut Tuncak, limekuja kabla ya mkutano wa kamisheni ya Umoja wa mataifa kuhusu haki za mtoto mjini Geneva.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni Tuncak ameeleza kwamba watoto wanazaliwa wameshaathirika kutokana na kukumbwa na chemikali za sumu tangu wakiwa tumboni.

Ripoti yake inaainisha pia takribani watoto 6000 kwenye mji wa Flint, Michigan, nchini Marekani wameathirika na kiwango kikubwa cha sumu kwenye maji ya kunywa, na jinsi dawa za kuua wadudu zinavyoendelea kuua au kujeruhi watoto walio katika ajira ya watoto au kula chakula kilicho kuwa na chemikali hizo.